Aliyekuwa Kamishna wa TRA Rished Bade
Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi kamishna wa mamlaka ya mapato TRA Bw.Rished Bade na kumteua Bw.Philiph Mpango kukaimu nafasi hiyo.
Taarifa kutoka ikulu zimesema kuwa uamuzi huo wa rais Magufuli umefuatia ziara ya waziri mkuu bandarini uliobaini upotevu wa makontena 349.
Aidha rais Magufuli amemtaka Rished Bade kutoa ushirikiano kwa Philiph Mpango wakati uchunguzi ukiendelea.
HELLOW!!! WELCOME THIS IS AMAxc THE GLOBAL MEDIA AND NEWS SUPPLIERS!!! amaxc.blogspot.com
Popular Posts
-
Duh hii ni aibu kwelikweli kuona msomi ambaye anategemewa kama kiongozi wa kesho kufanya mambo ya ajabu namna hii .. haya ni ...
-
Hii ni picha ya moja kati ya wanachuo msichana akiwa hosteli na ..demu huyo sio siri anawachanganya wengi chuo hapo ikiwemo ma lectur....
-
Mrembo mwenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye social media hapa Bongo, ambaye alishawahi kujinyakulia taji kubwa zaidi la ulimbwende hapa Bon...
-
Ikiwa leo ndio Uchaguzi wabunge wa Viti Maalum Kupitia Chama cha Mapinduzi Nchini katika Mkoa wa Singida Mgombea Wema Sepe...
-
Hz n baadh ya pcha za shilole akiwa na boy wake!! wakiwa kweny mapoz ya mahab ***** { clik here to see the video wakiwa wanaoga ...
-
john pombe magufuli Edward Ngoyai Lowassa. Uchunguzi uliofanywa na Timu ya Uwazi Mizengwe hivi karibuni na kuihusisha mikoa yote ya Ta...
-
Mwanamke aliye bambwa na sungusungu akifanya mapenzi kwenye kichaka na dereva wa teksi.Richard Bukos na Issa Mnally Mwanam...
-
Hzi n baadhi ya pcha za mastaa tofauti w KIKE hapa tz . sio siri n balaa coz sometmes najiuliza ! do they ril care???? ? ...
-
Kutoka kutangaza kutafuta mume Instagram hadi kukiri kumpenda Uhuru Kenyatta, Ray C anaendelea kutengeneza vichwa vya habari Afrika Masharik...
-
Blogu ya Wananchi Wednesday, August 19, 2015 TUJIKUMBUSHE HABARI KAMILI YA KAMATI TEULE YA BUNGE YA RICHMOND TAARIFA HII HAPA LIVE YA MWAKA ...
Friday 27 November 2015
breaking newzzz: rais john pombe magufuli amemsimamisha kaz kamishna mkuu TRA!!!clik here ujionee
Sunday 1 November 2015
amaxc blog: le babyzz aliyetikisa mitandao dis wikiendi...
imekuwa kawaida sana kuwachek mababyzz kwenye mitandao!!! such as insta, twitter na mingineyo miiingi
but huyu hapa ndo kauwa bendi wikiendi hii
unamjua n nani??????
stay tuned to amaxc..
amaxc blog: be ur own boss kwa kutumia nguvu kidogo tu!! kwa ufugaji kuku...
UFUGAJI WA KUKU WATANO (5) WA KIENYEJI
UPATE KUKU MIA MBILI (200) KWA MIEZI SITA
(6) TU!
(Kuku 200 x 5,000 = 1,000,000)
Unaweza ukaniona kama mimi ni kichaa na
ninaye ota ndoto za mchana ambazo hazina
mafanikio wala tija maana nadharia hii inaweza
isiwaingie vizuri watu vichwani mwao. Watu
wengi wamekuwa wakisema na kushauri hata
kushauriwa hata na wale wasiofaa. Ninaamini
wengi wetu hawapendi kuamini kile
wanachoambiwa hadi pale watakapoona kwa
macho yao ndipo waamini (akina Tomaso).
Sikia nikuambie! kama huamini haraka kitu
chochote hebu usimkatishe tamaa yule
aliyekwambia habari hizo za kukatisha tamaa,
badala yake jaribu kupeleleza na kufuatatilia
hatua kwa hatua tena kwa makini maelezo
uliyopewa, kisha yaweke katika utendaji
(tenda/fanya) kwa ufanisi kisha subiri
matokeo. Baada ya kupata matokeo sasa
unaweza kwenda mbele kidogo ukauliza/
kusoma/kujifunza zaidi ili kuona kama kuna
mahali umekosea au hukuzingatia kanuni na
maelekezo uliyopewa. Baada ya kupata
maelezo ya ziada hebu rudia kufanya tena kwa
kuboresha kupitia maelekezo ya awali na hayo
mapya uliyopata yote kwa pamoja ili upime
matokeo yake. Hapo sasa utakuwa upo
kwenye haki ya kuamini au kutoamini kwamba
jambo hilo ni kweli au siyo kweli na siyo kutaa
tu kwa ubishi usiokuwa na maana yeyote. Kwa
kufanya hivi hakika utapiga hatua mbele katika
kuboresha maisha yako ya sasa na ya baadae.
Ila ukifanikiwa usije ukamkufuru Mungu
aliyekuwezesha.
Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike
wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana).
Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula kilicho
na mchanganyiko kamili wa viini lishe
vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, yaani;
wanga, protini, calcium, chumvichumvi, madini
joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini).
Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/
kizungu/chotara (kama nilivyoeleza hapa chini
juu ya uchaguzi wa majogoo).
Wanapoanza kutaga watayarishie mahali
pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia
kwa kuwajengea viota ndani ya banda.
Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati
unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha
mahali hapo pana usalama wa kutosha (mahali
wanyama hatari kama vicheche, pakashume,
nyoka nk hawawezi kufika).
Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona
wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya
mayai unayotaka kuku wako walalie. Hii
inamaanisha kuwa; ukichagua mayai
makubwamakubwa hayo yanakuwa na
vifaranga majogoo na mayai madogomadogo
mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike. Acha
kuwawekea mayai ya mviringo kama mpira!
Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/
waatamie kwa pamoja.
Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku
1 kulingana na umbo la kuku wako. Kuku
anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila msimu
wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai
machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku
wako huku mayai mengine yakisubiri awamu
ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea
kuku wako hao watano, Kuku 5 x Mayai 12 =
Mayai 60.
Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa
siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa
vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku
walioatamia chakula chenye viini lishe vya
kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili
wakitoka kwenye viota vyao wale chakula
mara moja na kunywa maji kisha warudi
haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia
kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai
hata moja. Au hata yakiharikbika basi
hayataharibika mengi kama ukiacha
kuwawekea chakula waende kufukuzana na
panzi na vyakula majalalani huko nje na
kuchelewa kurudi kwenye mayai yao.
Wakati ukisubiria siku hizo 21/24 anza kujenga
kibanda kidogo ndani ya banda kubwa
ulilojenga awali au jikoni au andaa boksi kubwa
na gumu kwaajili ya kutunzia vifaranga
watakaoanguliwa ndani ya siku 21/24 zijazo.
Baada ya kuku hao 5 kuangua vifaranga wako
60 hapo ndipo kazi kubwa ya kulea vifaranga
inapoanza. Elewa kuwa ili upate mafanikio
haraka hakikisha kuwa kazi ya kulea vifaranga
inakuwa yako na siyo ya kuku! Kwanza,
Unatakiwa kuondoa na kuchoma moto/kufukia
mabaki yote ya mayai na kuboresha usafi wa
banda lote ili kuepusha magonjwa kama vile
kuharisha, viroboto, papasi nk. Hapo unaweza
kuwatoa vifaranga wako wote 60 mmojammoja
kadri wanavyoanguliwa hadi kufikia kifaranga
wa mwisho, yaani Yule wa 60 na kuwaweka
katika kibanda kidogo/boksi ulichokijenga na
kuwawekea mayai mengine mama zao (yale
15/18 kati ya 30 uliyoyabakiza) ili waatamie
tena kwa siku 21 hadi 24 zingine. Unapotoa
kifaranga kutoka kwa kuku aliyeatamia
humfanya kuku Yule ashindwe kutoka kwenye
mayai maana hana mtoto wa kulea.
Akimaliza kuangua mayai yote na ukamuwekea
mengine ni rahisi kwake kuendelea kuatamia
maana atasubiri kupata vifaranga na ndipo
atajikuta amelalia kwa siku 21 zingine bila
wasiwasi. Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari
umejipatia vifaranga/kuku zaidi ya 100 ndani
ya wiki 7 tu! Sasa Unatakiwa kuwajali sana
kuku hawa wanaolalia kwa mara ya pili kwa
kuwapa chakula cha kutosha, maji, majani ya
makongwe, mchicha, mchunga nk ili wapate
vitamini na madini mengine muhimu kwa afya
zao. Fanya hivyo hata watakapokuwa
wametotoa na ukawanyang’anya vifaranga. Hii
itawasaidia ili wasinyonyoke sana manyoya
maana kuku wengi hunyonyoka manyoya
wanapoatamia. Kwa kufanya hivi, kuku wako
watakaa kwa wiki 2 hadi 3 bila vifaranga na
kisha wataanza kutaga tena na kuatamia kama
mwanzo.
Vifaranga wako hakikisha unawatengenezea
chumba chao kido ndani ya banda kubwa/
jikoni, kisha wawekee chanzo chochote cha
joto kama vile; taa ya chemli/jiko la mkaa/
vizinga vya moto nk ili wasiathiriwe na baridi
hasa wakati wa usiku. Umakini mkubwa sana
unatakiwa hapa! Hakikisha unakuwa makini
wakati wa usiku ili kuongeza na kupunguza
joto ndani ya kibanda cha vifaranga maana
wakati huu maranyingi joto hupungua na
ubaridi huongezeka na hivyo unaweza kuua
vifaranga wako.
NAMNA YA KULEA VIFARANGA.
Katika ulezi wa vifaranga kama kuku
utawanyang’anya vifaranga vyao utatakiwa
kuwajengea banda dogo (ndani ya banda
kubwa/uzio) ili uwawekee chanzo cha joto
kama taa/jiko la mkaa (kama ni sehemu/
majira ya baridi). Kama utatumia jiko la mkaa
unatakiwa kuacha kwanza hadi mkaa mweusi
uwake wote ndipo uweke bandani maana mkaa
ukitoa moshi unaweza kuathiri vifaranga
vyako. Angalia namna ya kuweka jiko lako la
mkaa juu kidogo ili vifaranga wasiungue.
Hakikisha taa yako haitoi moshi sana na
haivujishi mafuta. Pia uwe na akiba ya mafuta
ya taa ya kutosha. Usiweke mafuta mengi
kwenye taa maana inaweza kulipuka ikakuletea
hasara. Vifaranga wasizidi 50 kwa boksi 1.
Hakikisha umewasha taa/jiko lako ndani ya
boksi saa tatu au zaidi kabla ya kuwaweka
vifaranga ili chumba/boksi lipate joto kabla ya
vifaranga kuwasili. Njia hizi zinahitaji uangalifu
wa hali ya juu sana kwani kuhatarisha/kuua
vifaranga ni kuhatarisha maendeleo yako.
Kama utaamua kutumia umeme pia ni vizuri
zaidi maana inapunguza hatari zaidi.
Kwa hiyoa njia zote tatu unaweza kutumia
jedwali lifuatalo ili kuweza kumeneji joto la
kibanda cha vifaranga;
UMRI WA KKUKU/VIFARANGAJOTO NDANI YA
BOX/KIBANDA CHA KULELEA
VIFARANGAJOTO NDANI YA CHUMBA/BANDA
Wiki 133-35oc30-32oc
Wiki 230-33oc27-29oc
Wiki 327-31c24-26oc
Wiki 424-29oc21-23oc
Wiki 526-27oc22-23oc
Baada ya wiki ya 4/5 pasua box/watoe kwenye
banda la kulelea ili walelewe kwa joto la
kawaida la banda/chumba.
Kwa kawaida joto hupimwa kwa kipimajoto
(thermometer), lakini kama huna kipimo hiki,
njia rahisi ni kuwaangalia kulingana na tabia
zifuatazo; Kama vifaranga wamejikusanya
sehemu moja basi joto ni kidogo bandani
mwao, au kama wanaenda mbali na chanzo
cha joto huku wanatanua mabawa yao na
wakihema harakaharaka basi joto ni kali/
limezidi kiwango. Pale watakapo tawanyika
vizuri ndani ya boksi/kibanda cha kulelea huku
wanakula na kunywa maji vizuri basi joto ni la
wasta na ndilo linalofaa. Kama unatumia njia ya
Boksi, basi unatikiwa kulipanua kulingana na
ukuaji na mahitaji ya vifaranga vyako.
Vifaranga wako wape chakula cha vifaranga
cha kutosha, maji safi na salama, majani
mabichi ambayo hufungwa kwa kuning’inizwa
kwa kamba,na CHANJO za minyoo nk ili
wapate vitamin, madini na protini itakiwayo na
kuzuia tabia ya kudonoana ili wakue vizuri.
Hakikisha kuwa chumba chao ni kisafi na
hakina unyevunyevu wakati wote.
Unyevunyevu husababisha ugonjwa wa baridi
na hufanya vifaranga wajikunyate na
kutetemeka na wanaweza kufa ghafla!
Inashauriwa kuwa siyo salama kufuga aina
nyingine ya ndege kama vile njiwa, bata, bata
mzinga nk kwa kuwachanganya na kuku
maana kila aina ya ndege wanamagonjwa yao.
Hivyo kuwachanganya kutakufanya ushindwe
namna ya kuwatibu wanapopatwa na ugonjwa.
Pia chawa wa njiwa huleta ugonjwa wa Ndui
hasa kuku wanapoangua vifaranga wao. Hapa
ugonjwa unaweza kufyeka vifaranga wako
wote 60/100 kama utafuata ushauri wangu!
Baada ya wiki 2 hadi 3 baada ya
kuwanyang’anya vifaranga kuku wako
wataanza tena kutaga mayai. Wakiatamia wote
5 Kama utaimarisha huduma kwao na kwa
vifaranga/kuku wale 100 tayari utakuwa una
kuku 105 au zaidi. Kuku wale 5 wa mwanzo
wakiatamia tena kwa siku 21 hadi 48 (kama
utafuata mfumo ule wa mwanzo wa
kuaatamishia mara 2) utajipatia vifaranga
wengine 100 tena na hivyo kuwa na kuku zaidi
ya 200 ndani ya miezi 5/6 tu! Ukiwahudumia
vifaranga wale wa mwanzo 100 vizuri kwa
miezi 3 na nusu nao wataanza kutaga kama
mama zao. kwahiyo, Chukulia walalie majike 5
wa mwanzo na majike 50 waliopatikana baada
ya uzao wa kwanza kwa miezi ile 3 ya mwanzo
utakuwa na mitetea 55. Wote wakiatamia na
watoe vifaranga 10 kila mmoja kwa siku
zilezile 21 hadi 46, tayari utakuwa na vifaranga
550! Sasa jumlisha na wale 150 waliobakia kati
ya kuku 200 na wote wakakua vizuri utapata
kuku na vifaranga zaidi ya 700! Jumlisha na
550 watakaototolewa na mama zao wale 5 wa
kwanza na wale 50 wa uzao wa 1 na 2 kwa
mara ya 2 si tayari utakuwa na kuku zaidi ya
1,200 ndani ya miezi 6 hadi 8 tu? Hivyo
utajikuta unao kuku zaidi ya 1,000!
Kati ya kuku 1,000 ukisema utoe kuku 800 wa
kuuza na ukiwauza kwa bei ya Tsh. 4,000 kwa
kila kuku 1 tayari utakuwa na Jumla ya Tsh.
3,200,000/= ambazo unaweza kufanya mtaji
wa mambo mengine au kuboresha mradi wako
zaidi. Unafikiri hapo hujaanza kufikia lengo la
kuku 1 akuletee shilingi Milioni 1? Ukiendelea
hivi inamaana kuku 1 atakuzalishia zaidi ya
hapo.
BANDA LA KUKU.
Unatakiwa kuwa na banda bora la kufugia kuku
ambalo litaweza kutunza kuku ili wasiweze
kupatwa na madhara mbalimbali kama vile;
kuliwa/kujeruhiwa na wanyama wakali,
kuchukuliwa na wezi nk. Lakini banda bora pia
litawasaidia kuku kuhimili mabadiliko
mbalimbali ya hali ya hewa yanayoweza
kujitokeza.
Sehemu ambayo inafaa kwa ujenzi wa banda
bora ni ile ambayo inaweza kufikika kwa
urahisi, iwe na mwanga wa kutosha, isiwe na
upepo mkali na isiyoruhusu maji kusimama au
kuingia ndani.
Banda ni vema likawa la ukuta/mbao/
mabanzi.matete/mianzi imara ili lishikilie paa
vizuri lisianguke. Kuta hizi zaweza kujengwa
kwa matofali ya saruji/matope/kuchomwa/
mabanzi/mbao nk. Katika kuezeka waweza
kutumia mabati/vigae/nyasi. Banda ni vema
likawa kubwa kulingana na kiasi cha kuku na
umri walionao. Kitu cha kuzingatia ni kwamba
banda liwe na hewa ya kutosha.
Kuku wanaofugwa ndani ni vema
wakatengenezewa uzio mpana (angalau Mita
8x10) ili wapate mahali wanapoweza kuota jua,
kupumzikia/kupunga hewa na kufanya mazoezi
(wawekee kamba/bembea/ngazi ndani ya
banda). Hakikisha kuwa banda ni imara na
hawatoki nje ya banda na kwenda mbali ili
uweze kuwawekea chakula cha kutosha na
maji na hata wale wanaotaga/kuatamia wapate
chakula na kurudi haraka.
Banda likiwa kubwa na bora litapunguza
magonjwa kwani litakuwa na hewa ya kutosha
ambayo itasaidia kupunguza joto na
unyevunyevu usio wa lazima bandani mwako.
Hii itasaidia uingizaji oksijeni ya kutosha na
kupunguza hewa chafu zenye madhara kwa
kuku. Pia litasaidia namna ya kufanya usafi
kwa urahisi na kupunguza vumbi ambalo
linaweza kusababisha kikohozi kwa kuku
wako. Ni vema banda lisipungue Mita 3 kwenda
juu.
Mambo muhimu ndani ya Banda.
Sakafu nzuri (iliyotengenezwa kwa saruji/
udongo ili isituamishe maji. Isiwe na nyufa ili
iweze kusafishwa kwa urahisi.
Hakikisha kuwa banda linakuwa na Viota
(vitagio) vizuri kwaajili ya kutagia. Viota viwe
na urefu wa Sentimita 30 na upana sentimita 30
na kina sentimita 35. Sehemu ya mbele izibwe
kwa sentimita 10 tu chini. Sehemu zote hizo
zizibwe kwa ubao. Kama kuku wako ni
wakubwa unaweza kuongeza upana, urefu na
kina kiasi cha kutosha mfano, Upana na Urefu
35cm, kina 55cm nk. Hakikisha kiota/kitagio
kinakuwa na giza kiasi maana kuku hupenda
kutaga mahala pa giza kidogo/palipojificha.
Giza litasaidia kuku asiweze kula mayai au
asiweze kudonoana na kuku wengine. Kiota pia
kinatakiwa kiwe mahali ambapo ni rahisi kwa
kuku kuingia na kutoka, pia iwe ni rahisi
kusafisa.
Ndani ya kiota kuwekwe majani makavu/
maranda ya mbao laini na kinyunyize dawa ya
unga ya kuzuia viroboto/utitiri kabla ya kuweka
nyasi.
AIDHA, ni vizuri sana kuwawekea kuku
wanaoatamia mayai wakati wa usiku maana
ukimuwekea wakati wa mchana anaweza
kuyaacha.
Kuku anayetarajiwa kuatamia ni vema
akachunguzwa kama anao utitiri/viroboto/
chawa kwenye manyoya yake. Wadudu hawa
humkosesha raha kuku anayeatamia na wengi
huacha mayai na kukimbia/wasitulie kwenye
viota vyao. Hali inapelekea kuanguliwa kwa
vifaranga wachache. Unaweza kumuona
mtaalam wa mifugo kwa ushauri zaidi.
Banda liwe na vichanja maana kuku hupenda
kulala juu ya vichanja maana nao ni ndege.
Vyombo safi na vizuri kwaajili ya chakula na
maji.
Walazie majani makavu/maranda ya mbao/
makapi ya mazao sakafuni kwa banda zima.
UCHAGUZI NA UHIFADHI WA MAYAI.
Mayai huharibika kwa urahisi sana yasipo
tayarishwa na kutunzwa vizuri kwa uangalifu.
Matayarisho huanzia bandani hadi ndani kwa
kufanya yafuatayo;
Hakikisha viota vyote ni safi wakati wote.
Chakula kiwe ni cha kuimarisha gamba la yai
na vyakula vingine.
Vyombo vya kukusanyia mayai viewe safi na
imara.
Kusanya mayai mara2 hadi 3 kwa siku ili
kuepuka mayai kuvunjwa/kuliwa/kuchafuka
kwa mayai mengi na kupoa haraka.
Ondoa mayai yaliyo na nyufa na maganda
yasiyo imara.
Safisha mayai mara baada ya kukusanya na
kabla ya kuweka kwenye chombo cha
kuhifadhia saa 12-24. Mayai yanaweza
kuoshwa kwa maji ya uvuguvugu (nyuzijoto
35oc) na kusugua taratibu kwa mkono ili
kuondoa uchafu (kama upo). Lakini
unashauriwa kusugua kwa mkono bila maji ili
kusafisha maana maji hupunguza ubora wa yai
na maranyingi yai huharibika haraka.
Weka katika vyombo visafi kwa kuelekeza
sehemu ya yai iliyo pana iwe juu na sehemu
nyembamba iwe chini, beba kwa uangalifu.
Hifadhi mayai katika sehemu ya baridi
nyuzijoto10 hadi 16 za sentigredi.
Mayai yapangwe kwa daraja kwa kufuata
ukubwa na rangi ili kuvutia wateja na kuongeza
bei. Pia unaweza kuweka kwa kufuata muda
unapoyaokota kutoka bandani. Weka lebo
yenye tarehe ili usichanganye wakati wa
kuwaatamishia kuku wako/kuuza.
Kuchagua mayai ya kuatamishia kuku kwaajili
ya kuangua vifaranga.
Mayai yanayofaa kwa kuatamiwa na
kuanguliwa ni vema yawe na ukubwa wa
wastani, yasiwe na ufa/nyufa, yasiwe ya
mviringo kama mpira, yasiwe na uchafu
wowote juu ya gamba lake, yasiwe
yametengwa kwa zaidi ya wiki 1 (siku 7).
NJIA MBALIMBALI ZA UFUGAJI WA KUKU.
Kuna njia kuu mbili za ufugaji wa kuku.
Ufugaji Huria
Aina hii ya ufugaji, kuku huachiwa huru
wajitafutie chakula na maji wao wenyewe.
Utaratibu huu hutumika zaidi kufugia kuku wa
kienyeji ambapo mfugaji hupata hasara na
pengine hupata faida kidogo maana kuku
hukosa uangalizi na hawapewi chakula cha
ziada.
Faida.
Haina gharama kubwa za ufugaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)