Popular Posts

Wednesday 28 October 2015

amaxc blog: sentensi tano za mbowe akizungumza na waandishi wa habari trh 27 oktoba liveeee

Ni saa chache tu baada ya kuanza kutangazwa kwa matokeo ya Urais ya mwaka 2015 Tanzania ambapo leo October 27, 2015 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kazungumza na waandishi wa habari. ‘Yako mambo mengi yanatendeka ya hujuma dhidi ya mgombea wetu LOWASSA ili asishinde kiti cha urais, sambamba na kujaribu kupunguza kwa nguvu isipokuwa halali idadi ya wabunge wa UKAWA kwa kutumia jeshi la polisi’- MBOWE ‘Leo ni siku ya tatu jeshi la polisi limewaweka ndani vijana wetu wa IT zaidi ya 100, huku wengine wakifikishwa mahakamani, Kwahiyo wao wenzetu wamejaribu kuvunja mfumo wetu wa mawasiliano, wametumia polisi kuharibu vifaa vyetu vya kuhesabia kura’ – Mbowe .l ‘Katika mifumo kama hiyo tunapata wakati mgumu sana kuamini kwamba tume inachokifanya pamoja na serikali yake kina nia njema kwa nchi yetu‘ – Mbowe

Friday 23 October 2015

amaxc blog: mbalon kwa kumtusi raisi jakaya na mwanae...

Mkazi wa mjini Moshi, Kyefa Joachim Makundi (33), leo amepandishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka ya kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Mbali na shitaka hilo, mshitakiwa huyo amesomewa shitaka lingine la kumtukana Ridhiwan Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze anayemaliza muda wake. Mshitakiwa huyo amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga na kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Agatha Pima. Wakili Pima amedai mahakamani kuwa Oktoba 17 mwaka huu katika baa ya Harambee iliyopo katikati ya mji wa Moshi, mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Kikwete na mwanae Ridhiwan. Ingawa matusi hayo hayakuandikwa kwenye hati ya mashitaka, lakini wakili Pima amedai kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 89(1) (a) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002. Chini ya kifungu hicho, mtu yeyote anayetumia lugha ya matusi, kuudhi, au kudhalilisha dhidi ya mtu mwingine katika hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani anatenda kosa la jinai. Adhabu inayotolewa kwa mtu anayepatikana na hatia katika kosa hilo ni kifungo cha miezi sita jela. Hata hivyo, mshitakiwa amekana shitaka hilo ambapo mahakama imesema dhamana ilikuwa wazi ikiwa mshitakiwa atakuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh1.5 milioni kila mmoja. Source: Mwananchi

Saturday 17 October 2015

Friday 16 October 2015

amaxc blog: Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania October 17 na 18

<Michezo: Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania October 17 na 18 
 By team leader
 on October 16, 2015
 113 shares
... Baada ya mapumziko ya Ligi mbalimbali duniani ili kupisha mechi za kalenda ya FIFA kumalizika, weekend hii Ligi Kuu mbalimbali zinaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, huenda ukawa unataka kufahamu mechi za weekend hii zitakazochezwa za Ligi Kuu Tanzania Bara, Uingereza na Ligi Kuu Hispania hii ndio ratiba ya mechi za weekend hii. Ligi Kuu Tanzania bara mechi za October 17 na 18 vpl
Mechi zote za Ligi Kuu Tanzania bara zitachezwa saa 16:00 kwa saa za Afrika Mashariki Mechi za Ligi Kuu Uingereza weekend ya October 17 na 18
EPL
 Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Uingereza kwa saa za Afrika Mashariki 
 Tottenham Vs Liverpool saa 14:45 Chelsea Vs Aston Villa saa 17:00 
 Crystal Palace Vs West Ham saa 17:00 Everton Vs Man United saa 17:00 Man City Vs Bournemouth saa 17:00 Southampton Vs Leicester City saa 17:00
 West Brom Vs Sunderland saa 17:00 Watford Vs Arsenal saa 19:30 
 Jumapili ya October 18
 Newcastle Vs Norwich saa 18:00
 Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Hispania
LALIGA
 Ratiba za mechi za Hispania kwa saa za Afrika Mashariki
 Real Madrid Vs Levante saa 17:00 
 Eibar Vs Sevilla saa 19:15
 Barcelona Vs Rayo Vallecano saa 21:30 Valencia Vs Málaga saa 23:00
 Real Betis Vs Espanyol saa 23:05 
 Mechi za Jumapili ya October 18 Villarreal Vs Celta de Vigo saa 13:00
 Real Sociedad Vs Atl Madrid saa 17:00 Getafe Vs Las Palmas saa 19:15 Deportivo de La Coruña Vs Ath Bilbao saa 21:30

amaxc blog: Ndoa ina miaka 10, kumbe Nameless na Wahu waliwahi kuchokana? Kilichofuatia je?

Entertainment; Ndoa ina miaka 10, kumbe Nameless na Wahu waliwahi kuchokana? Kilichofuatia je? Ni raha kuwa na Familia, mtu na mke wake wote mnafanya kazi Industry moja halafu wote mnafanya poa na watu wanakubali kazi zenu.. hiyo ni raha sana kiukweli !! Pata picha Jay Z na Beyonce wake.. Lakini moja ya Familia ya mastaa walioteka soko la muziki East Africa, Nameless na Wahu ni mfano mzuri wa mastaa ambao wamedumu kwenye Ndoa yao kwa miaka 10 na wote wanafanya muziki… “Ndoa sio kitu rahisi, mnatakiwa kusomana na kila mmoja amkubali mwenzake vile alivyo… mnatakiwa kuheshimiana pia” >>> Hii ni nukuu ya alichokisema David Mathenge aka Nameless, staa wa muziki Kenya na mume wa Wahu. Wahu
Wahu na mmoja wa watoto wao. “Kuna wakati mimi na Wahu tunachokana, na najikuta nasema kwamba sikuhitaji tena na yeye anasema hivyo hivyo hataki kuniona tena…. Lakini mara nyingi tunaenda kwa washauri halafu mambo yanakuwa sawa… Tulianza uhusiano tukiwa wadogo sana wakati huo tuko Chuo… Tulipendana, tukakua pamoja.. Tumetafuta maisha pamoja na kwa sasa tuna msingi mzuri sana wa maisha yetu” >>> Nameless. Wako mastaa ambao wanaamini wakioa au kuolewa wanajiongezea majukumu na kufanya washuke kimuziki, unaweza kucheki mfano mzuri kwa hawa watu wetu wa +254, ndoa miaka 10 na wako pazuri tu !!

amaxc blog: Hii ndio Hospitali ya kwanza kufunguliwa kitengo cha kuhudumia Wanaume waliobakwa !!

Duniani: Hii ndio Hospitali ya kwanza kufunguliwa kitengo cha kuhudumia Wanaume waliobakwa !! Kesi za wanawake kubakwa au kudharirishwa kijinsia ni kitu ambacho kimesikika sana.. lakini ishu za matukio ya wanaume kubakwa sio stori ambazo zimesikika sana au kuzoeleka masikioni mwa wengi !!
Hii Hospitali imeangalia pia umuhimu wa kutoa huduma kwa wanaume ambao wamebakwa au kufanyiwa ukatili wa kijinsia, ni Hospitali ya Södersjukhuset ambayo iko Jiji la Stockholm, ndani ya Sweden. Uongozi wa Hospitali hiyo wameweka Kitengo cha Huduma ya Dharura kwa ajili ya kuhudumia Wanaume waliobakwa, Huduma kwenye Hospitali hiyo zinatolewa kwa saa 24 na kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili…
Mmoja wa Viongozi wa Serikali alielezea umuhimu wa Huduma hiyo >>>>”Nadhani hii ni Kliniki ya kwanza Duniani, tumefanya Utafiti Mitandaoni na hatujaona kama kuna sehemu nyingine inatoa Huduma ya aina hiyo… Wanaume wote watahudumiwa bure kabisa… Ni matumaini yetu kwamba waathirika wengi wa matukio ya aina hiyo ambao huwa wanajificha, watajitokeza kuhudumiwa“ Huduma hii inaonekana kuwa na umuhimu wake kwa Wanaume wa Sweden, Takwimu zinaonesha kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2010 Sweden iliongoza kwenye Takwimu za matukio ya Wanaume kubakwa katika Nchi za Ulaya

amaxc blog: VIFO SABA VYA TAIFA WAKATI HUU WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MUNGU AWAWEKE PEMA PEPONI!! AIMEEEN!!

1. Mohamed Mtoi, - UKAWA
 2. Celina Kombani, - CCM 
3. Abdallah Kigoda,- CCM
 4. Christopher Mtikila, - UKAWA
 5. Estomihi Malla, - ACT-WAZALENDO
 6. Emmanuel Makaidi, - UKAWA
 7. Deo Filikunjombe. - CCM ****mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi!! amen!!!

BREAKIN NEWZZ!!:- PICHA ZA KWANZA 10 ZA HUZUNI ZA KIFO CHA MBUNGE WA CCM LUDEWA NA WENZAKE JINSI MABAKI YA MIILI YAO YALIYVOPATIKANA HUKO MBUGANI SELOUS/IRINGA

LIVE!!
Chopa aliyokuwa akiitumia wakati wa Uchaguzi Mbunge wa CCM Ludewa Marehemu Deo Filikunjombe, chopa iliyomletea mauti jana usiku.
Marehemu Deo Filikunjombe
mungu azilaze roho za marehem mahala pema pepon!. ameen