Michezo:
Lionel Messi anusurika kupelekwa mahakamani, baba yake anaweza kufungwa miezi 18 jela…

Unaikumbuka ile kesi ya Lionel Messi na baba yake mzazi Jorge Messi kutuhumiwa kukwepa kodi? basi stori kutoka mtandao wa the42.ie kuhusu muendelezo wa kesi hiyo baada ya waendesha mashitaka nchini Hispania kuona Lionel Messi hana Kesi ya kujibu ila baba yake anayo kesi ya kujibu.

Lionel-Messi-goals-Season-201516
Ripoti kutoka mtandao huo unaeleza kuwa waendesha mashitaka wa Catalunya wameona Lionel Messi hana kesi ya kujibu ila baba yake Jorge Messi itamlazimu kutumikia kifungo cha miezi 18 jela kama akikutwa na hatia ya kosa la ukwepaji kodi. Lionel Messi na baba yake walikuwa wakituhumiwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha euro milioni 4.1 kati ya mwaka 2007 hadi 2009.
Lionel-Messi-Jorge-Messi

Lionel Messi na baba yake Jorge Messi
Jorge Messi ambaye ni baba wa Lionel Messi ana tuhumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi, kwani yeye ndio muhusika mkuu wa tukio hilo ambaye huwa anasimama kama wakala wa Lionel Messi katika shughuli zake mbalimbali. Lionel Messi kwa sasa yupo nje ya uwanja kwa muda wa wiki nane akiuguza jeraha lake
No comments:
Post a Comment