Popular Posts

Friday 22 July 2016

BELLA KUWEKA HISTORIA LEO DODOMA>> KUKIWASHA ROYAL VILLAGE.....



BELLA KING of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ leo anatarajiwa kuweka historia kwa kufanya bonge moja la shoo ndani ya Ukumbi wa Royal Village, Dodoma.

Akizungumza na Mtandao wa Global Publishers mratibu wa shoo hiyo, Renatus Gregory alisema kuwa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni shoo ya kihistoria sambamba na sapraizi kibao.
“Njooni tuweke historia pamoja ambapo kutakuwa pia na DVD za maisha ya Bella kimuziki kwa muda wa miaka 10 tangu aingie nchini.
“Shoo itakuwa ni ya Live
kwa kutumia vyombo, nina imani mashabiki watafurahia kwani pia Malaika Band itaambatana na Bella,” alisema Renatus.
Mashabiki watatakiwa kulipia kiingilio kiduchu cha shilingi 30,000 kwa VIP na kawaida shilingi 10,000.
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook

No comments:

Post a Comment