Popular Posts

Sunday 19 July 2015

AMAxc BLOG: BEEF LA WEMA NA ANT EZEKIEL TENA KIMENUKA!!!!! JIONEE SABABU

URAFIKI wa mashaka! Mastaa wawili wa filamu
Bongo, ambao walikuwa mashosti kwa muda
mrefu kabla ya kidudumtu kuingilia kati hivi
karibuni na kusuluhishwa, hivi sasa bifu kati
yao limeanza upya, Risasi Mchanganyiko
linakujuza.
Chanzo chetu ambacho hakipepesi macho
kinasema tangu Aunt ajifungue mtoto, Wema
hakuwahi kukanyaga nyumbani kwake kwa ajili
ya kumuona, kutoa hongera au hata pole kwa
rafiki yake huyo, isipokuwa wamekuwa
wakichati kupitia simu za mikononi, kitu
ambacho si sahihi.
Lakini kali zaidi, ni kitendo cha Wema
kushindwa kuhudhuria sherehe ya kutimiza
siku 40 tangu azaliwe mtoto huyo, Cookie, kitu
kilichomfanya mwenzake kumuondoa kabisa
katika orodha ya marafiki zake.
“Yaani Aunt kipindi chote alimvumilia akijua
huenda yuko ‘bize’, lakini kwa kutofika kwenye
siku hiyo muhimu, amemtoa kabisa akilini
mwake,” kilisema.
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili
lilimtafuta kwa njia ya simu Aunt ili kuthibitisha
ubuyu huo, lakini akakubali tu juu ya
kutohudhuria kwenye tukio hilo muhimu la
mtoto wake, licha ya kuwa alimpa taarifa.
“Hakuja, lakini siwezi mlaumu sana, labda
alikuwa na majukumu mengi, ukizingatia hivi
sasa ana mambo ya ubunge,” alisema.
Wema hakuweza kupatikana baada ya simu
yake kutopokelewa kwa muda wote
alipopigiwa.

No comments:

Post a Comment