Popular Posts

Saturday 18 July 2015

AMAxc BLOG: COSTAL UNION KUKIPIGA KESHO IDD PILI NA FRIENDS CORNER!!!!!

MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania
bara mwaka 1988 Coastal Union ya Tanga
kesho Iddi Pili inatarajia kucheza mechi
ya kirafiki na timu ya Friends Corner
ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu
mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Iddi Pili
kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa
ni muendelezo wa mechi za kujipima
nguvu kwa ajili ya kukiimarisha kikosi
hicho kwa ajili ya mashindano ya Ligi kuu
yajayo.
Maandalizi ya kuelekea mechi hiyo
yamekamilika kwa asilimia kubwa na
hivyo Friends Corner watatua mkoani siku
hiyo hiyo ya mchezo huo tayari kwa ajili
ya mchezo huo.
Taarifa inaeleza baada ya kumalizika
mechi hiyo tutaangalie uwezekano wa
kucheza mechi nyengine za majaribio ili
kuweza kukipa makali kikosi cha timu
hiyo ambacho msimu ujao kimedhamiria
kuleta mapinduzi kwenye michuano hiyo.
Na mtambue kuwa dhamira ya timu yetu
ni kuhakikisha inafanya maandalizi
kabambe ili kuweza kurejesha heshima yao
ya miaka ya nyuma walipochukua
ubingwa wa ligi kuu.
Hata hivyo tunawataka wanachama,
wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa
wingi kwenye mechi hiyo ili kuweza kuona
viwango vya wachezaji wapya
waliosajiliwa kabla ya kuanza msimu
mpya wa Ligi kuu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Coastal Union.
OSCAR ASSENGA.

No comments:

Post a Comment