Popular Posts

Sunday 19 July 2015

AMAxc BLOG: MH JAKAYA ARUDI NYUMBANI TZ BAADA YA KUTOKA USWIZI KIKAZI!!!!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na mfanyakazi wa Shirika la Ndege la
Uswisi katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam mara baada ya kurejea nyumbani
baada ya ziara ya kikazi mjini Geneva
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam mara
baada ya kurejea nyumbani baada ya
ziara ya kikazi mjini Geneva. PICHA NA
IKULU
Akiwa mjini Geneva, Rais Kikwete
ameongoza vikao vya  Jopo la Kimataifa
Linalopendekeza Jinsi Dunia inavyoweza
kukabiliana na majanga yajayo ya
magonjwa ya milipuko ambalo kazi yake
imeungwa mkono na nchi 21 ambazo
zilichangia mapambano dhidi ya ugonjwa
wa Ebola.
Miongoni mwa mikutano ambayo
Rais Kikwete ameiongoza katika Makao ya
Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva ni
pamoja na yeye na wanajopo wenzake
kutoa maelezo kuhusu maendeleo ya kazi
yao kwa nchi ambazo zilichangia
mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola
katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra
Leone.
Nchi hizo ambazo zimeunga mkono
kazi ya Jopo hili katika mkutano huo ni
Venezuela, Umoja wa Ulaya (EU), Uholanzi,
Finland, Shirikisho la Russia (Russian
Federation), Norway, China, Ubelgiji,
India, Ujerumani, Marekani, Uswisi,
Canada, Brazil, Denmark, Uingereza,
Israel, Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), Umoja wa Afrika (AU), Benki ya
Dunia (WB), Jamhuri ya Korea na Japan.
Pamoja na kwamba wajibu mkuu
wa Jopo hili siyo kuchunguza ugonjwa wa
Ebola na madhara yake, bado ugonjwa
huo ni msingi mkuu wa kazi ya Jopo hilo
ambalo wajibu wake ni kutumia uzoefu wa
Ebola kutoa mapendekezo ya jinsi dunia
inavyoweza kukabiliana na majanga ya
magonjwa ya milipuko katika siku zijazo.
Ugonjwa wa Ebola ambao ulilipuka
katika nchi hizo tatu za Afrika Magharibi
mwishoni mwa mwaka 2013 mpaka sasa
umeua watu 11,000 katika nchi hizo na
kusababisha mshtuko mkubwa duniani.
Hiyo ilikuwa mara ya 24 kwa
ugonjwa huo kulipuka katika Afrika tokea
ulipolipuka kwa mara ya kwanza mwaka
1976, miaka karibu 40 iliyopita, katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
wakati huo ikiitwa Zaire.
Hata hivyo, katika milipuko ya
kwanza 23, ugonjwa huo uliua watu
wachache zaidi kuliko mlipuko wa 24.
Jopo hilo limeambiwa kuwa tofauti
na matarajio ya dunia kuwa ugonjwa huo
ulikuwa unamalizika katika nchi hizo
hasa katika Liberia, umeanza kupata kasi
tena na nchi hizo tatu zinakisiwa kuwa na
wagonjwa karibu 70.
Jopo hilo lenye Wajumbe sita
liliteuliwa Aprili, mwaka huu, na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa
Ban Ki Moon na kufanya vikao vyake vya
mwanzo Mei, mwaka huu, katika makao
makuu ya UN, mjini New York, Marekani.
Mbali na kukutana na nchi
zilizochangia mapambano dhidi ya Ebola,
Rais Kikwete na Jopo lake limepata nafasi
ya kumsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi wa
Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya
Afrika, wakati ugonjwa huo unalipuka Dkt.
Luis Gomes Sambo wa Angola ambaye
aliwaeleza wajumbe historia ya ofisi ya
kanda hiyo iliyoko mjini Brazzaville,
Jamhuri ya Congo, katika kukabiliana na
ugonjwa huo.
Aidha, Wajumbe wa Jopo
wamemsikiliza Mkurugenzi mpya wa
Kanda, Dkt. Matshidizo Rebecca Moeti
ambaye amezungumza kwa njia ya
mkutanomtandao (teleconference) kutoka
mjini Brazzaville. Dkt. Moeti alianza kazi
yake Januari Mosi, mwaka huu, 2015.
Vile vile, Wajumbe wa Jopo
wamesikiliza jitihada za Jamhuri ya
Rwanda kukabiliana na magonjwa ya
mlipuko kupitia kwa Waziri wa Afya wa
nchi hiyo, Agnes Binagwaho ambaye naye
alizungumza kwa mkutanomtandao
kutoka Kigali, Rwanda.
Nje ya vikao hivyo, Rais Kikwete
alikutana na kufanya mazungumzo na
Katibu Mkuu Mstaafu wa UN, Mheshimiwa
Kofi Annan. Katika mkutano huo kwenye
Hoteli ya Intercontinental, viongozi hao
wawili wamezungumzia masuala mbali
mbali ya kimataifa, ikiwamo hali ya
Burundi.
Rais pia amekutana kwa
mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kituo
cha South Centre ambacho kina makao
yake mjini Geneva, Dkt. Martin Kohr. Kituo
hicho kilianzishwa chini ya uongozi wa
Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kwa nia
ya utekelezaji wa Ripoti ya Kamisheni ya
Nchi Zinazoendelea (South-South
Commission), ambayo iliongozwa na
Mwalimu.

No comments:

Post a Comment