Popular Posts

Saturday 25 July 2015

BREAKING NEWS!!!!LOWASA ATAJA SIKU RASMI YA KUHAMIA CHADEMA!!!!!

Zipo tetesi kwamba Edward Lowasa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari Jumapili tarehe 26 Julai 2015 Jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo, Lowasa anatarajiwa kueleza mambo mengi juu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM uliopelekea jina lake kukatwa.

Pia katika mkutano huo, Lowasa anatarajiwa kutangaza rasmi kujivua
uanachama wake ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA ambapo baadaye jioni ataelekea viwanja vya Mwembeyanga ambako ataungana na viongozi wengine wa CHADEMA kwenye mkutano wa hadharaza. Mtakumbuka kuwa uwanja huo wa Mwembeyanga uliopo Temeke Dar es Salaam ulitumika kutaja orodha ya mafisadi 11 na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa mwaka 2007 ambapo jina la Lowasa lilikuwa miongoni mwa majina yaliyopo kwenye orodha hiyo. 

BOFYA HAPA KUSOMA YOTE

No comments:

Post a Comment