Popular Posts

Thursday 30 July 2015

AMAxc BLOG: KAMA UNATABIA HIZI HUWEZI KUFANIKIWA KWENYE MAISHA YAKO!!!!!

1. KUMSIKILIZA KILA MTU
Kama kila anayekuambia kitu kuhusiana na
unachofanya unamsikiliza nakuhakikishia hutopiga
hatua kubwa. Katika jambo lolote unalofanya kuna
watu watakutia moyo na kuna wengine
watakukatisha tamaa. Wapo watakaokwambia
haiwezekani au huwezi. Tena wanaokwambia
haiwezekani watakupa mpaka mifano ya
walioshindwa. Kama unataka kufikia mafanikio
makubwa acha kuwasikiliza watu wanaokukatisha
tamaa, chagua ni kitu gani unatafanya na anza
kukifanyia kazi mpaka ufikie mafanikio yako.
2. UNAFANYA KILE AMBACHO KILA MTU
ANAFANYA
Huwezi kuamini ila iko hivi, mafanikio makubwa
yanakuja pale ambapo unakwenda hatua ya ziada.
Kwenye kila unachofanya kuna hatua ya ziada
ambapo kama ukienda hatua hiyo utafikia
mafanikioa makubwa sana. Kama unaamka asubuhi,
unakwenda kazini, unafanya kazi ulizopangiwa, jioni
unarudi nyumbani, unalala na kesho unarudia tena
huo mzunguko sahau kuhusu mafanikio makubwa.
Kama unafanya biashara kama kila mtu
anavyofanya kwa mtindo huo huo na mbinu hizo
hizo ambazo kila mtu anayefanya biashara hiyo
anatumia unasogeza siku tu. Kama unataka kufikia
mafanikio makubwa NENDA HATUA YA ZIADA.
Kama unaishi maisha ya bwana mike utasubiri sana
na hutofikia mafanikio makubwa.
3. UNATUMIA MUDA HOVYO
Poteza milioni mia moja, unaweza kuzitengeneza
tena baada ya muda fulani, poteza sekunde moja
ndio umeisahau kabisa. Hakuna kitu chenye
thamani zaidi ya muda, lakini ndio tunautumia
kizembe kuliko kitu chochote kile. Ili uweze kufikia
mafanikio makubwa lazima uweze kuwa na
matumizi mazuri ya muda wako. Tunaishi kwenye
dunia yenye kelele nyingi, kuna vyombo vya habari,
simu, email, mitandao ya kijamii na maongezi
mengine yanayokusubiri wewe kila siku. Usipokuwa
makini unaweza kuona unakwenda na wakati
kumbe unakwenda nje ya mstari wa mafanikio.
kitabu kava tangazo
4. UNAPENDA MAJIBU YA HARAKA
Sijui ni kitu gani kimeharibu dunia kwa sasa ila
kizazi cha sasa kinapendelea majibu ya haraka
kuliko vizazi vivlivyopita. Unataka uanze biashara
leo na mwezi ujao uwe umetengeneza faida mara
mbili ya mtaji!! Yaani unataka upande mchungwa leo
na wiki ijayo uanze kula machungwa. Hakuna kitu
kama hicho ndugu yangu, mambo mazuri yanahitaji
subira na yanahitaji uvumilivu. Usidanganyike na
kelele unazopigiwa na watu kwamba fanya hivi
utafikia mafanikio ya haraka, hayo ni matangazo ili
kufaidisha biashara zao. Huwa napenda kutumia
mfano huu mara kwa mara, huwezi kuwachukua
wanawake tisa ukawabebesha ujauzito mmoja
ndani mwezi mmoja wakatoa mtoto, kama unatafuta
njia ya mkato ya kufikia mafanikio unaweza
kuyapata ila hutofika mbali.
5. UNA MATUMIZI MABOVU YA FEDHA ZAKO
Hili nalo linatabia ya kushangaza sana. Ukiangalia
kwa makini, waliofanikiwa kifedha wana matumizi
tofauti kabisa na wale wanaolalamika kutokuwa na
fedha kila siku. Wakati wale wenye fedha nyingi
wakitafuta sehemu za uwekezaji, wale wanaozipata
kidogo wanatafuta viwanja vya kuzitumbua. Hata
kama unapata fedha kidogo kiasi gani ni lazima uwe
na kiwango ambacho uaweka pembeni. Jilipe wewe
kwanza kwenye kila kipato unachopata na hii
itakusaidia kuweza kuwa na maisha yasiyo na hofu
juu ya fedha. Kujua zaidi jinsi ya kujilipa wewe
kwanza soma makala hii unamlipa kila mtu kasoro
huyu mmoja wa muhimu

No comments:

Post a Comment