Popular Posts

Friday 31 July 2015

AMAxc BLOH: HATIMAYE BRAZA WAKE ZARI AMCHUMBIA LINNAH!! JIONEE HAPA

Mbongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ na mchumba wake ambye ni kaka za Zari, Wiliam Bugene ‘Boss Mtoto’. Hatimaye staa wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amechumbiwa rasmi na yule jamaa wake, Wiliam Bugene ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka kiukoo wa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.’
Akizungumza na Amani kwenye mahojiano maalum alipotimba katika Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Zanzibar hivi karibuni, Linah alisema kuwa ana furaha maishani mwake kwa kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye atafunga naye ndoa ‘soon’.
“Tayari ameshanichumbia, anajulikana kwetu na mimi najulikana kwao. Kifuatacho ni ndoa yangu,” alisema Linah ambaye hivi karibuni amesema ataachia wimbo mpya utakaokuwa gumzo. Furaha ya Linah inakuja kufuatia kumpata mwanaume huyo ambaye amekuwa akionekana naye kila kiwanja wakiwa wamegandana kimahaba ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipodai kuporwa bwana’ke, Nagari Kombo anayedaiwa kakwapuliwa na Wema Sepetu. Kabla ya Boss Mtoto na Kombo, huko nyuma Linah aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye uchumba ‘serious’ na msanii mwenzake, Amini Mwinyimkuu.
SOURCE:GPL

No comments:

Post a Comment