Mteule wa kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu ujao, John Pombe Magufuli na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape NNauye wakipiga ngoma.
WAKATI mteule wa Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu ujao, John Pombe Magufuli akifahamika kama mtu makini kwenye utekelezaji wa majukumu yake, imethibitika kuwa waziri huyo wa Ujenzi pia ni mkali kwenye upigaji wa tumba, Risasi Jumamosi linakupa zaidi.
Hali hiyo imefahamika baada ya gazeti hili kuchimbua matukio mbalimbali ambayo yamemuonyesha mbunge huyo wa Chato akipiga tumba kwa umahiri mkubwa kiasi cha kuwaacha hoi watu wengi.
Mathalan, katika uzinduzi wa daraja la Mbutu, wilayani Nzega mkoa wa Tabora, uliofanyika Januari 7, 2013, Magufuli alionekana akipiga Tumba wakati bendi kongwe ya Msondo Ngoma ikitoa burudani katika hafla hiyo, akiwa sambamba na wanamuziki wa kundi hilo, Shaaban Dede na Hassan Moshi ‘TX Jr.
Licha ya siku hiyo, pia kwa nyakati tofauti Magufuli alionyesha umahiri wake katika kupiga Tumba katika hafla mbalimbali, kama vile wakati wa ziara ya Rais Jakaya Kikwete mkoani Kagera, alipojiunga na kundi la uhamasishaji na burudani la chama hicho tawala, kwa kukitendea haki kifaa hicho cha muziki.
Aidha, wabunge wawili wa upinzani, John Mnyika (Ubungo) na Halima Mdee wa Kawe, watakuwa ni mashuhuda wa uhodari wa Magufuli, kwani katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Msewe- Baruti iliyofanyika miezi michache iliyopita, mteuliwa huyo wa CCM aliifanya tena shughuli hiyo mbele ya umati wa wananchi waliohudhuria.
Aidha, hivi karibuni wakati akitambulishwa kwa wanachama wa chama hicho kama mgombea wake katika Viwanja vya Zakheem, Mbagala jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Magufuli pia alipiga tumba kwa umahiri wa hali ya juu kabla ya kuhutubia mamia ya wanachama hao.
Mwanamuziki mmoja kutoka bendi moja kubwa nchini aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema Magufuli ni mkali na anaweza kuwafunika wapigaji tumba wengi nchini.
HELLOW!!! WELCOME THIS IS AMAxc THE GLOBAL MEDIA AND NEWS SUPPLIERS!!! amaxc.blogspot.com
Popular Posts
-
Duh hii ni aibu kwelikweli kuona msomi ambaye anategemewa kama kiongozi wa kesho kufanya mambo ya ajabu namna hii .. haya ni ...
-
Hii ni picha ya moja kati ya wanachuo msichana akiwa hosteli na ..demu huyo sio siri anawachanganya wengi chuo hapo ikiwemo ma lectur.... ...
-
Mrembo mwenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye social media hapa Bongo, ambaye alishawahi kujinyakulia taji kubwa zaidi la ulimbwende hapa Bon...
-
Ikiwa leo ndio Uchaguzi wabunge wa Viti Maalum Kupitia Chama cha Mapinduzi Nchini katika Mkoa wa Singida Mgombea Wema Sepe...
-
Hz n baadh ya pcha za shilole akiwa na boy wake!! wakiwa kweny mapoz ya mahab ***** { clik here to see the video wakiwa wanaoga ...
-
john pombe magufuli Edward Ngoyai Lowassa. Uchunguzi uliofanywa na Timu ya Uwazi Mizengwe hivi karibuni na kuihusisha mikoa yote ya Ta...
-
Mwanamke aliye bambwa na sungusungu akifanya mapenzi kwenye kichaka na dereva wa teksi.Richard Bukos na Issa Mnally Mwanam...
-
Hzi n baadhi ya pcha za mastaa tofauti w KIKE hapa tz . sio siri n balaa coz sometmes najiuliza ! do they ril care???? ? ...
-
Kutoka kutangaza kutafuta mume Instagram hadi kukiri kumpenda Uhuru Kenyatta, Ray C anaendelea kutengeneza vichwa vya habari Afrika Masharik...
-
Blogu ya Wananchi Wednesday, August 19, 2015 TUJIKUMBUSHE HABARI KAMILI YA KAMATI TEULE YA BUNGE YA RICHMOND TAARIFA HII HAPA LIVE YA MWAKA ...
Saturday, 18 July 2015
AMAxc BLOG: KUMBE Mh MAGUFURI NI MKALI WA HIZI!!!!!!!
Labels:
amaxc™
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment