Popular Posts

Saturday, 18 July 2015

AMAxc BLOG: WEMA SEPETU AMUANGUKIA KAJALA!!! BIFU LAO KWISHNEY!!!!!!!

Staa wa filamu za bongo, Wema Sepetu ‘Madam’.
HAKUNA mwanzo usiyokuwa na mwisho! Huu ni usemi pekee ambao umejidhihirisha kwa Mkurugenzi wa Endless Fame Production na mbunge mtarajiwa wa Viti Maalum mkoani Singida kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu baada ya kumwangukia aliyekuwa shostito wake, Kajala Masanja ‘Kay’.
Wema na Kajala wamekuwa na bifu zito lililokuwa likichukua sura mpya kila kukicha kufuatia wawili hao kutokusameheana, kutukanana na kukashifiana ambapo Wema alifikia hatua ya kumwita mwenzake ‘bogasi’ na yeye (Kajala) akamwita chizi.
Tukio la Wema kujishusha na kutoa kauli ya kusema yuko tayari kumsamehe Kajala aliitoa mbele ya mwandishi wetu, Julai 15, mwaka huu ndani ya Ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Kajala Masanja ‘Kay’.

No comments:

Post a Comment