Popular Posts

Friday, 17 July 2015

HII NDO PICHA YA KWANZA KURUSHWA YA SAYARI PLUTO

Picha hiyo imepigwa na chombo kisicho na
binadamu kilichotumwa kwenye safari hiyo
ambacho kilisafiri umbali wa kilometa bilion saba na
tano.
Chombo hicho jana jumanne kilitua kwenye sayari
hiyo.
Katika mkutano na waandishi wa habari katika chuo
Kikuu cha Johns Hopkins kilichopo Maryland
Marekani, Mkuu wa utafiti wa sayari hiyo Alan Stern
hakusita kuonyesha furaha yake.
"Jana ilikuwa ni siku nzuri na ya kipee kwangu, vipi
kwenu."
Mkuu huyo wa utafiti Alan Stern amesema chombo
hicho cha anga kimekusanya taarifa nyingi kutoka
kwenye sayari hiyo.
"Sawa chombo chetu cha New Horizons
kimekwenda sasa zaidi ya mile milioni moja.
Zaidi ya kilometa moja na nusu upande wa pili wa
Pluto, hivyo ndivyo tunavyokwenda kwa haraka
tumefikia karibu na sayari hiyo hapo jana asubuhi.
Chombo chetu cha anga kipo katika hali nzuri,
kinafanya mawasiliano na dunia kwa mara nyingine
mara kwa mara kwa masaa kuanzia asubuhi saa 11
na dakika 50.
Tayari tumepata data kutoka kwenye vifaa vya
kisayansi vipatavyo vitano, na tutatoa taarifa
kuhusu matokeo tuliyopata, lakini ukweli ni kwamba
tunachunguza

No comments:

Post a Comment