Popular Posts

Monday 21 September 2015

amaxc Beki aliyemvunja mguu Luke Shaw wa Man United, kafanya faulo nyingine ya hatari.. (+Pichaz&Video)

Michezo: Beki aliyemvunja mguu Luke Shaw wa Man United, kafanya faulo nyingine ya hatari.. (+Pichaz&Video)
Ikiwa ni wiki moja imepita toka beki wa klabu ya Manchester United, Luke Shaw avunjike mguu wake wa kulia, baada ya kufanyiwa tackling na beki wa klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi Hector Moreno, tukio lililopelekea kutolewa uwanjani katika dakika 15 za mwanzo.
Hii ni faulo aliyomfanyia Luke Shaw katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hector Moreno ameingia tena katika headlines ya kucheza faulo mbaya, ambayo ingeweza kumvunja Oussama Tannane wa klabu ya Heracles. Moreno ambaye alimfanyia tackling Luke Shaw na kumvunja mguu wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Ulaya amefanya faulo ya hatari kwa Oussama
Tannane. Hii ni faulo aliyomfanyia Oussama Tannane Beki huyo wa PSV amecheza faulo hiyo dakika ya 72 ya mchezo, baada ya kushindwa kuumiliki mpira mrefu uliyopigwa kutokea upande wa Heracles kuelekea langoni kwao hivyo Moreno na Oussama Tannane wote walikuwa na asilimia 50 kwa 50 ya uwezekano wa kila mmoja wao kuupata mpira ila Moreno akamkang’anyaga juu ya ugoko Oussama Tannane

No comments:

Post a Comment