Popular Posts

Tuesday 15 September 2015

amaxc blog: Sergio Aguero kuukosa mchezo wa kwanza wa UEFA!!!! na hawa n wachezaj walio rejea uwanjan wakitokea majeruh!!!!! kaz ipo...

Klabu ya Manchester City ya Uingereza September 15 inashuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza ya hatua ya makundi ya klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya klabu ya Juventus ya Italia, hii ndio mechi ya kwanza ya kundi D kwa klabu zote mbili.
Sergio Aguero Manchester City wamethibitisha kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeitumikia klabu hiyo Sergio Aguero baada ya kupata majeraha ya goti. Aguero ataukosa mchezo dhidi ya Juventus baada ya kupata majeraha ya goti katika mechi dhidi ya Crystal Palace, mechi iliyomalizika kwa Man City kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
David Silva Mshambuliaji huyo alipata jeraha la goti baada ya kufanyiwa tackling na Scott Dann hivyo hatokuwepo katika mechi hiyo, pamoja na hayo kocha wa klabu hiyo Manuel Pellegrini amethibitisha kurejea kwa David Silva na Raheem Sterling licha ya kukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace.
Raheem Sterling

No comments:

Post a Comment