Popular Posts

Saturday 5 September 2015

amaxc blog: super star jackline wolper aanika ukaribu wake na lowassa!!!! jioneee mwenyew live!!!!

KIKAANGONI Leo ni safu mpya ambayo inampa msomaji wa gazeti hili kumuuliza staa yeyote wa Bongo kuhusu suala analohitaji ufafanuzi.Kwa kuanzia leo, staa anayefungua safu hii kwa kujibu maswali ya wasomaji ni nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper. Swali kubwa ambalo alitumia muda kulifafanua ni ukaribu wake na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye anaungwa mkono na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa. Swali: Mimi nataka kujua, Wolper ana ukaribu gani na Edward Lowassa wa Ukawa maana wengine wanasema ni mtu wake wa karibu sana. 0718 817616. Wolper anajibu: “Mimi na Lowassa hatuna ukaribu wa zaidi ya kumkubali kisiasa tu. Napenda utendaji kazi wake. Ndiyo maana popote anapokwenda niko naye.” ***** Swali: Mimi swali langu kwa dada Wolper. Je, kwa sasa ameolewa? Na kama hajaolewa, naweza kupata nafasi ya kupeleka posa kwa mzee Masawe? 0654 763789.Wolper anajibu: “Mimi sijaolewa. Kama unajiaminisha kuleta barua kwa baba yangu fuata taratibu.” Swali: Najua Wolper amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyabiashara Dallas, wakamwagana. Je, bado wanawasiliana na Dallas yuko wapi? 0758 211153.Wolper anajibu: “Mimi na Dallas ni mtu na rafiki yake kwa sasa. sijui yuko wapi lakini naamini anaendelea vizuri huko aliko.” ***** Swali: Kuna madai kwamba, Wolper kwa sasa unatoka kimapenzi na mfanyabiashara mmoja mkubwa Bongo. Je, ni kweli? Kama si kweli, kwa sasa unatoka na nani? 0673 626094. Wolper anajibu: “Mh! Siwezi kumwanika hapa. Lakini siku itafika atajulikana tu. Teh! Teh! Teh!” ***** Swali: Wolper kuna rafiki yako mmoja aliniambia gari unaloendesha kwa sasa pia umehongwa na mwanaume mmoja. Tena mume wa mtu. Je, unaliongeleaje hilo? 0717 272313. Wolper anajibu: “Mh! Si kweli. Nilishaumwa na nyoka kuhusu kuhongwa magari na sasa sitaki tena. Kama kweli nimehongwa, mwenye ushahidi ajitokeze hadharani.”

No comments:

Post a Comment