
Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal na klabu ya
Sabah ya Malaysia EL Hadji Diouf ameingia kwenye
headlines baada ya siku kadhaa nyuma kuandikwa
katika kitabu kipya cha kiungo wa kimataifa wa
Uingereza anayeichezea klabu ya LA Galaxy ya

Marekani Steven Gerrard.
EL Hadji Diouf aliingia katika headlines ya kitabu
hicho ambacho ni cha maisha ya Steven Gerrard
na kikubwa kilichomfanya azungumziwe ni baada
ya Gerrard kuzungumzia ndani ya kitabu hicho

kuwa angalau EL Hadji Diouf ndio aliwahi
kumpenda.
El Hadji Diouf
Stori ni kuwa EL Hadji Diouf hajaichukulia poa kauli
ya Gerrard na hajafurahishwa nayo hata kidogo
kwani kauli kama hiyo kwa upande wa EL Hadji
Diouf ameichukulia tofauti na kusema kiungo huyo
wa LA Galaxy ni mbaguzi wa rangi kwani
inamaanisha hakuwahi kuwapenda wachezaji
wengine weusi waliyowahi kusajiliwa na Liverpool .
Steven Gerrard akiwa ameshika karatasi yenye
ujumbe wa kupinga ubaguzi wa rangi.
“Gerrard hakuwahi kuwapenda watu weusi, kila
wakati nilipokuwa na pishana nae hakuwahi
kuthubutu kuniangalia machoni”>>> El Hadji Diouf
Steven Gerrard na EL Hadji Diouf ni wachezaji
ambao wamewahi kucheza pamoja katika klabu ya
Liverpool ya Uingereza kati ya mwaka 2002 hadi
mwaka 2005, ambapo EL Hadji Diouf alihama
Liverpool na kujiunga na klabu ya Bolton
Wanderers kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment