Popular Posts

Monday 21 September 2015

amaxc blog: ETHIOPIA imeanza rasmi kutumia treni ya abiria inayo tumia umeme!!! jionee bonge la hatua hili mtu wangu!!!

Duniani: Ethiopia wameanza rasmi kutumia Treni za abiria zinazotumia umeme..
Nimepita kwenye page ya Facebook ya BBC Swahili nikakutana na hii stori ambayo nimeguswa kuishare hata hapa amaxc blog ..kuhusu nchi ya Ethiopia kuzindua Treni za umeme.
3Ripoti inasema Treni hizi ambazo zimezinduliwa September 20 2015 zinaanza kubeba abiria na zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa watu kwenye mji mkuu wa Addis Ababa, Ethiopia nchi ambayo mpaka mwaka huu wanasema idadi ya watu wake ni zaidi ya MILIONI 90.
BBC wanasema hizi Treni zimetajwa kuwa mfano na za kwanza kusini mwa jangwa la sahara ambapo ujenzi na uendeshaji wa huduma hii ya reli unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya China.
Picha zote ni kutoka BBC.
Treni hizi za umeme zitakua na uwezo wa kuhudumia Abiria elfu kumi na tano ndani ya dakika 60 ambapo Treni moja inaweza kubeba abiria 286 kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment