Popular Posts

Tuesday 22 September 2015

amaxc blog: Watu Milioni 2 wamejitokeza kuomba kazi India, unajua nafasi zilitolewa ngapi?

General News: Watu Milioni 2 wamejitokeza kuomba kazi India, unajua nafasi zilitolewa ngapi? Takwimu zinaonesha China inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu Duniani ambapo ina jumla ya watu Bilioni 1.38, nafasi ya pili ni India ambayo ina jumla ya watu Bilioni 1.31, hao sio watu wachache mtu wangu kwa sababu ukiangalia Dunia nzima ina jumla ya watu Bilioni 7 !! Tatizo la ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa sana sasahivi kila sehemu Duniani, nchi ya India inaingia kwenye stori kubwa kwa leo… ishu ni kwamba Serikali ya India ilitangaza nafasi 368 za kazi kwa Walinzi pamoja na Wahudumu wa Chai Maofisini, lakini unaambiwa kwenye nafasi hizohizo 368 watu waliojitokeza kuomba nafasi walikuwa watu Milioni 2.3. Wengi walioomba kazi wanasema walipoona tangazo ilibidi watume maombi kwa sababu hakuna ajira na maisha ni magumu. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa, UN zinaonesha mpaka kufikia mwaka 2030 India itaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, ikifuatiwa na China na Marekani

No comments:

Post a Comment