Popular Posts

Saturday 19 September 2015

amaxc blog: maamuz ya UKAWA baada ya chama pinzan kukiuka taratibu za kisheria!!! ....

Siasa: Maamuzi ya UKAWA baada ya chama pinzani kukiuka taratibu za kisheria….
Ni headlines za Uchaguzi mwaka 2015 ambapo leo Sept 18, Mwanasheria wa CHADEMA ambaye ni mkuu wa idara ya Uchaguzi kwenye sheria,Bw.John Mallya alifanya mkutano wa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu uki ukwaji wa sheria na chama pinzani. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari..’Ndugu waandishi wa habari tumewaita hapa hususani mambo ya kisheria yanayoendelea kwenye kampeni zoezi la uchaguzi ni zoezi la kikatiba, sheria ya uchaguzi wa taifa mwaka 1985 kanuni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na maadili ya uchaguzi wa Ubunge, Urais na Udiwani pamoja na sheria nyingine ikiwemo ya rushwa na sheria ya vyama vya kisiasa – John Mallya
.
‘Sheria kwa mfano ambayo ni maadili ya Uchaguzi ya mwaka huu vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu kupitia makatibu wake wakuu wameweka sign zao inakataza kwa mfano suala la mtu kutoa bango la mtu mwingine lakini chadema imepata hiyo changamoto kwamba mabango yake wameondolewa kwa mfano hili bango lipo Nyerere Road pale Mwanza limeondolewa na watu wa CCM ilikuwa ni nyumbani ya mtu binafsi wakamtishia watachoma nyumbani yake wakamrushia mawe wakavunja vioo vyake na baada wakaliondoa‘ – John Mallya .
‘Na hii inaonesha sio tu ni namna gani CCM sio tu wamekiuka sheria lakini hawafai kutawala nchi kwasababu suala la kuweka bango ni suala la kisheria ukiona bango la Samia,Magufuli na mtu yoyote limewekwa kisheria‘ – John Mallya
. ‘Mabango, sera, vipeperushi vyote vinakuwa vimesajili na tume ya Uchaguzi kwa madhumuni ya Kampeni kwa mfano ujumbe wa Mabadiliko umesajiliwa na nembo ya CHADEMA pia imesajiliwa, sasa CCM wanakiuka sheria wame ku copy na ku paste wanachukua ilani na sera zetu ambapo wamechukua nembo yetu M4C ambayo sisi tunaita Movement 4 Change huku CCM wakiwa wanasema M4C ni Magufuli 4 Change‘ – John Mallya
Waandishi wa Habari. ‘Katika hili tumechukua hatua nzito kuliko hizi za mwanza maana yake hili sio la kimadili hili ni uvunjwaji wa sheria, Chadema tunampeleka Magufuli Mahakamani pamoja na bodi ya wadhamini wa chama cha Mapinduzi‘ – John Mallya

No comments:

Post a Comment