Popular Posts

Sunday 20 September 2015

amaxc blog: je unamkumbuka livaldo wa FC BARCELONA?? kafanyiwa upasuaji..jionee here liveee

Michezo: Unamkumbuka Rivaldo wa FC Barcelona? Kafanyiwa upasuaji taarifa ipo hapa… (+Picha)
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Brazil Rivaldo bado dunia ya soka ina mkumbuka kwa umahiri wake uwanjani lakini amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’or mwaka 1999. Mwaka 2004 aliingia katika list ya wachezaji bora 100 wa FIFA waliohai.
Rivaldo ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil waliotwaa Kombe la Dunia 2002, kwa sasa ni Rais wa klabu ya Mogi Mirim na amepost picha katika mtandao wa kijamii inayoonyesha amefanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia, hivyo hiyo ni ishara ya kuwa upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio.
Rivaldo na mtoto wake mwaka 2003 Hata hivyo licha ya Rivado kustaafu soka bado yupo mbadala wake yaani mwanaye Rivadinho amefuata nyayo za baba yake na anacheza soka, kuna wakati waliwahi kuingia katika headlines ya kucheza pamoja katika klabu ya Mogi Mirim na wote kufunga magoli. Rivaldo kwa sasa ana umri wa miaka 43.
Rivaldo wakati yupo FC Barcelona ya Hispania

No comments:

Post a Comment