
Tunamfahamu kama bwana afya, na hii ni kutokana
na uwezo aliojaliwa Muumba wa kuweza kula
mpaka mifupa. Wengi wetu hatufahamu gharama
anayoipata fisi kutokana na kuwa na uwezo huo wa
kula mifupa, kwato mpaka pembe za wanyama
wengine. Ni kwamba, Mfumo wa mmeng'enyo wa
fisi una tindikali ambazo ndizo zinampa kiburi
mnyama huyu kupambana na mifupa iliyowashinda
wenzie. tindikali hizi hufanya kazi ya kumeng'enya
bidhaa zote ambazo Fisi huzitupiamo kinywani
mwake. Zoezi la kumeng'enya mifupa na vyakula
vingine huishia kuzalisha joto kali sana kwenye
mwili wa fisi. Endapo fisi hatachukua hatua stahiki
joto lile linaweza kupanda na kufikia viwango vya
hatari vyenye kuweza kuhatarisha maisha yake.
Joto huwa kali kiasi cha kuweza kuanza kuharibu
baadhi ya viungo vyake vya ndani.
ili kuweza kukabiliana na joto hilo na pia kunusuru
maisha yake, fisi hulazimika aidha kutafuta mahali

ambapo kuna kivuli au Sehemu yenye maji au Tope.
Sehemu hizi ndizo ambazo Fisi atazitumia kujaribu
kupunguza makali ya joto ili lisimletee madhara
zaidi. Chaguo la namna ya kujihifadhi hutegemea na

mazingira aliyopo. Mathalani kwa fisi hawa
tuliowakuta ndani ya Hifadhi ya Serengeti
walilazimika kujitosa kwenye matope yaliyokuwa
kandokando ya barabara ya Serengeti- Ngorongoro.
hii ni kwasabu eneo ambalo tuliwakuta fisi hawa,
hakukuwa na kichaka au mti wa kuweza kuwapa
kivuli kizuri kupumzika. Hali hii hupelekea pia fisi
kupenda kufanya mawindo yake usiku ambako hali
ya joto huwa ni ya chini. Jua la mchana na shibe ni
mateso kwa bwana afya.
No comments:
Post a Comment