Popular Posts

Tuesday 18 August 2015

amaxc blog: madereva kugomesha usafiri takriban siku 5 hiv...!! jionee kisa

Chama cha Wafanyakazi Madereva nchini Tanzania (TADWU) kimetangaza rasmi kusitisha huduma za usafiri kwa madereva kuanzia wiki ijayo kwa kipindi cha siku tano ama zaidi kwa madai kwamba madereva watakuwa wote katika mafunzo yanayolenga kuwafundisha namna ya kuzuia ajali zinazotokana na uzembe wakati wakiwa barabarani. Naibu Katibu Mkuu wa (TADWU), Bw. Rashid Salehe amesema madereva wote wakiwemo wa mabasi ya abiria watalazimika kusitisha huduma kwa kuwa watakuwa wakishiriki mafunzo hayo ambayo yanatokana na elimu waliyopewa viongozi wa chama hicho wakati wa mkutano kati yao na Wizara ya Kazi na Ajira.

No comments:

Post a Comment