Popular Posts

Tuesday 18 August 2015

amaxc blog: Man City na Valencia wamefikia hapa kuhusu usajili wa Nicolas Otamendi...

Michezo Man City na Valencia wamefikia hapa kuhusu usajili wa Nicolas Otamendi Klabu ya Manchester City ya Uingereza bado inaendelea kusajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Uingereza kwani baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu kumtaka beki wa kati wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya Valencia ya Hispania Nicolas Otamendi wamefikia makubaliano.
Nicolas Otamendi huenda akatua katika jiji la Manchester wakati wowote kuanzia hivi sasa baada ya kuachwa na Valencia katika kikosi kitakachokutana na Monaco katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa UEFA August 19, vyombo vya habari vingi vinaripoti staa huyo aliyejiunga na Valencia akitokea FC Porto ya Ureno 2014 atajiunga na Man City wakati wowote kuanzia hivi sasa.
Hata hivyo mpango huo wa kumsajili Nicolas Otamendi kwenda Man City umefikia makubaliano kwani klabu ya Man City imekubali kulipa pound milioni 31.7 kama ada ya uhamisho ya nyota huyo ila katika makubaliano hayo pia inamuhitaji Eliaquim Mangala kwa mkopo kama sehemu ya kukamilisha uhamisho wa Nicolas Otamendi kwa mujibu wa vyombo vingi vya habari vya Hispania.

No comments:

Post a Comment