Popular Posts

Friday 21 August 2015

amaxc blog: mfahamu mnyama mzito kuliko wote duniani!!!!

NYANGUMI WA BLUU AU the blue whale ni mnyama aishie baharini na ana urefu wa mita 30 na uzito wa kilo hadi 201,000 au tani 210 na zaidi,ni mnyama mkubwa na mzito kuliko yeyote aliyewahi kutokea duniani. HAYA NI MAMBO MATANO UNATAKIWA UYAJUE KUHUSIANA NA MNYAMA HUYU mkubwa duniani. 1:NYANGUMI WA blue alikuwa anapatikana karibu katika bahari zote duniani mpaka mwanzoni mwa karne ya 20,ambapo walianza kuwindwa na wawindaji haramu mpaka jumuia ya kimataifa ilipoamua kulinda WANYAMA HAO mwaka 1966.
2:NYANGUMI WA BLUE hula zaidi wanyama wadogo wa baharini wanaoitwa KRILL_na nyangumi mmoja hula zaidi ya Krill milioni 40 kwa siku_hivyo inabidi waishi katika maendeo yenye msongamamo mkubwa wa wanyama hao
3:NYANGUMI JIKE HUZAA MTOTO MMOJA KILA BAADA YA miaka miwili au Mitatu…na mototo wa nyangumi akizaliwa huwa na uzito wa tani 3 na urefu wa mita 7_na hunyonya maziwa ya mama yake lita 500 na zaidi au gallon 150 kwa siku
4:Wanasayansi wanakadiria kuwa NYANGUMI WA BLUE huishi hadi miaka miaka 80
5:UZITO WA ULIMI wa nyangumi wa blue ni sawa na uzito wa tembo mmoja

No comments:

Post a Comment