Popular Posts

Saturday 29 August 2015

amaxc blog: manuel pellegrin amethibitisha kumkosa kiungo huyu!!!!! kwasababu hii...

Michezo Manuel Pellegrini athibitisha kumkosa nyota huyu kwa sababu hii……. Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Manchester City ya Uingereza Wilfried Bony August 28 amepost picha katika mtandao wa Instagram inayomuonesha akiwa anatembelea magongo huku mguu wake ukiwa umevalishwa kiatu maalum cha plastic kwa ajili ya majeraha aliyoyapata katika mguu wake wa kushoto.
Wilfred Bony alijiunga na klabu ya Manchester City akitokea klabu ya Swansea City kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 28. Kocha wa klabu ya Man City Manuel Pellegrini amethibitisha kumkosa mchezaji huyo katika mechi ya kesho dhidi ya Watford.
“Kwa bahati mbaya Bony alipata majeraha jana hivyo hatokuwepo katika mchezo wa kesho na huenda akawa nje ya uwanja kwa siku saba hadi kumi”>>> Manuel Pellegrini

No comments:

Post a Comment