Popular Posts

Friday 21 August 2015

amaxc blog:pigo kubwa kwa vyama vya siasa jijini dar!!! unajua imekuwaje???! jionee hapa

Jiji la Dar es Salaam limepiga marufuku maandamno yeyote ya vyama vya siasa hasa wakati wa kampeni na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa chama au wafuasi wowote watakaobainika kufanya maandamo hayo. Agizo hilo kali kwa wafuasi na vyama vya siasa imekuja siku moja tu kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi mkuu, ambapo kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam vyama vyote vya siasa na wafuasi wao watakaofanya kampeni zao Dar es Salaam hawanabudi kuachana na dhana ya maandamo kuelekea kwenye viwanja vya mikutano kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Kwa upande wa jeshi la polisi wanasema wako imara katika kutekeleza agizo hilo na kwamba hawatovumilia chama au kikundi chochote kitakacho sababisha uvunjaji wa amani katika kipindi cha kampeni. Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka watendaji katika mitaa kutokukubali watu watakaokufa kwa kipindupindu kuzikwa na ndugu zao kwani inaweza kuwa chanzo cha kuzidi kusambaza ugonjwa huo. Kwa mujibu wa maafisa wa afya wanasema ugonjwa huu wa kipindupindu wakati wa kiangaza husambaa haraka zaidi, huku ulaji vyakula vilivyopoa, kutokunawa mikono vizuri, ulaji hovyo wa matunda vikitajwa kuwa moja ya sababu za ugonjwa huo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoitoa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mpaka sasa kuna wagonjwa 36 wa kipindu pindu huku wagonjwa wapya wakiwa 9 ambapo kata zilizo athirika zaidi zikiwa ni Mwananyamala, Manzese, Saranga, Kimara, Ubungo,Kigogo, Tandale na Kijitonyama. Via>>>ITV

No comments:

Post a Comment