Popular Posts

Wednesday, 5 August 2015

amaxc blog: hatimaye kikwete amesaini miswaada iliyo kuwa ikigomewa na wapinzani!!! n ballaa tupu

Rais Jakaya Kikwete amesaini miswada ya sheria mitano ikiwemo mswada wa sheria mafuta, mswada wa sheria wa sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pamoja na mswada wa sheria wa uwazi na uwajibikaji iliyopitishwa katika bunge lililopita. Awali akizungumza katika halfa ya kusaini miswada hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambayo imehudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali akiwemo makamu wa rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, makatibu wakuu pamoja na waziri, katibu mkuu kiongozi Dkt Ombeni Sefue amesema sheria hizo zinajibu mahitaji na changamoto zilizokuwa zinawakabili wananchi katika sekta ya mafuta na gesi, mahitaji ya walimu pamoja na mahitaji ya wakulima pamoja na kuiweka Tanzania sehemu nzuri kimfumo. Akitoa maelezo kabla ya rais kuisaini mswada wa mafuta pamoja na mswada wa uwazi na uwajibikaji, waziri wa nishati na madini, Mhe, George Simbachawene amesema miswada hiyo inalenga kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asili na kusisitiza pamoja na kuwepo kwa miongozi ya sera na sheria kuhusu shughuli za mkondo wa juu, wakati na wachini wa mafuta na gesi asili nchni bado miongozo hiyo inakabiliwa na matatizo mbalimbali yanayotokana na ukuaji wa sekta ndogo ya mafuta na gesi pamoja na mabadiliko ya tasnia ya mafuta na gesi. Kwa upande wake akitoa taarifa fupi ya mswada wa usimamizi wa mapato yatokanayo na mafuta na gesi pamoja na mswada wa sheria ya masoko ya bidhaa kabla ya Mhe. Rais kuisaini, waziri wa fedha Mhe.Saada Mkuya amesema hadi kufikia may 2915 kiasi cha gesi kilichopatika bahari na nchi kavu ni futi za ujazo trilioni 55.08 kiasi ambacho fedha zitakazopatikana kupitia gesi hiyo kitainufaisha Tanzania kimapato na kuimarisha uchumi. Aidha akitoa taarifa fupi ya mswada wa sheria ya tume ya walimu, waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dkt Shukuru Kawambwa amesema serikali kwa kuzingatia umuhimu wa walimu nchni imeamua kurudisha tume ya walimu nchni itakayoshugulikia walimu wa shule ya msingi na sekondari ambayo iliyovunjwa baada ya maboresho yaliyofanyika katika sekta ya utumishi wa umma.

No comments:

Post a Comment