Popular Posts

Wednesday, 12 August 2015

amaxc blog: hii hapa kali na mpya kutoka japan!! mawasiliano bila kuonana!!!! jionee vituzzzz hapa

Japan wamekuja na style mpya ya kuwasiliana kupita mitandao, ni mawasiliano bila kuonana sura…ungependa kujua inakuaje? Japan National Institute of Informatics imekuja na teknolojia mpya ya miwani inayoitwa “Privacy Glasses”. Hii ni miwani inayoweza kuuficha uso wako mbele ya camera zozote na pia ni miwani yenye uwezo ya kuficha uso wa mtu mbele ya mashine yoyote.
 Ubunifu huu unaiwezesha miwani hiyo kufyonza mwanga wowote unaoipiga miwani hiyo na pia kuwezesha kuuficha uso wa mtu mbele ya camera au computer yoyote ile, kizuri zaidi ni kwamba majaribio yaliofanyika yametoa majibu chanya kwa asilimia 90% ya bidhaa hiyo. Watengenezaji wa miwani hii wamesema bidhaa hiyo itapatikana sokoni mwezi wa 6 mwakani kwa dola 240 (Tzs. 480,000/=).

No comments:

Post a Comment