
Kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu Ujerumani
Bundesliga August 1 imepigwa mechi ya Fainali ya
Super Cup, mchezo huo ulizikutanisha timu za FC
Bayern Munchen dhidi ya klabu ya Wolfsburg
katika uwanja wa Volkswagen Arena.
Mchezo umemalizika kwa Wolfsburg kuibuka
washindi baada ya dakika 90 za mchezo
kumalizika kwa sare ya goli 1-1, hadi dakika ya 88
FC Bayern Munchen walikuwa wanaongoza kwa
goli 1-0 goli lililofungwa na Arjen Robben dakika ya
47 ya mchezo kabla ya Nicklas Bendtner kufunga
goli la kusawazisha dakika 89 kwa upande wa
Wolfsburg .

mchezaji kevin de bruyne akiibuka na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
Hivyo ikalazimika kupigwa mikwaju ya penati
ambapo Wolfsburg wakaibuka na ushindi kwa jumla
ya penati 5-4 kwa upande wa FC Bayern Munchen
kiungo wa Kihispania Xabi Alonso alikosa penati.
Sambamba na hayo kiungo wa kimataifa wa
Ubeligiji Kevin De Bruyne alipata tuzo ya mchezaji
bora wa mwaka inayotolewa na waandishi wa
habari za michezo Ujerumani.
Pichaz na Video nimekusogezea mtu wangu








clik hapa uone mechi ilivyo kuwa
No comments:
Post a Comment