Popular Posts

Tuesday, 11 August 2015

amaxc blog: vurugu tupu kura za maoni ccm zahesabiwa kituo cha polisi!!! unajua wap hyo?? klik hapa

Vurugu na malalamiko ya uchaguzi wa kura za maoni za udiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Kahangara wilayani Magu mkoa wa Mwanza, vimesababisha matokeo yake kutangaziwa katika kituo cha polisi. Matukio ya vurugu na malalamiko kama hayo yamekuwa yakitokea katika maeneo mengi nchini baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa ubunge na madiwani. Baadhi ya wafuasi wa CCM waliokuwa wameandamana kupinga matokeo yaliyompa ushindi, Deus Machibula, diwani aliyemaliza muda wake, walisema hawakubaliana na matokeo hayo kutokana na uchaguzi kutawaliwa na vurugu na rushwa. Hata hivyo, wana-CCM hao waliokuwa wamebeba mabango mbalimbali yaliyokuwa yameandikwa ujumbe tofauti yakiwamo yaliyosomeka,Tunamtaka Mussa Samson diwani wa kata ya Kahangara kwa maendeleo ya wote. Mmoja wa mawakala wa mgombea Samson, Joel Ally, alisema chanzo cha vurugu na matokeo kutangaziwa kituo cha polisi ni viongozi wa CCM kata na wilaya kushindwa kutenda haki kwa wagombea wote kitendo kilichosabisha baadhi ya wananchi na wana CCM waliochoswa na viongozi mzigo, kufanya fujo. Ally alisema uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa wazi wazi na upendeleo pamoja na fomu za kupigia kura kuchakachuliwa, wajumbe kupiga kura mara tatu kinyume cha kanuni na taratibu za uchaguzi wa chama. “Mawakala wa Samson hatufahamu namna Machibula alivyoibuka mshindi, hatuelewi kabisa na hatukubaliani na matokeo hayo yaliyotangaziwa kituo cha polisi na mawakala hatukupewa taarifa,” Ally. Katibu wa CCM kata ya Kahangara, Cravery Makologoto, alithibitisha kuwapo kwa vurugu hizo na matokeo hayo kutangazwa polisi ni kutokana na wafuasi wa Samson kusababisha vurugu. Hata hivyo, licha ya kudaiwa kuongoza katika uchaguzi huo wa kura za maoni, lakini Machibula hajatangazwa licha ya kudai kuaminiwa na wana-CCM kuwaletea maendeleo katika kata hiyo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa hakupatikana kuzungumzia taarifa hizo kutokana na simu yake kutokuwa hewani hadi tunakwenda mitamboni.

No comments:

Post a Comment