Popular Posts

Wednesday, 12 August 2015

amaxc blog: hii ndo sababu iliyo mtoa rafael da silva man united, van gaal anahusika??!!! jionee full story.

Ikiwa zimepita siku kadhaa toka aliyekuwa beki wa pembeni wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Rafael da Silva aondoke klabuni hapo na kutimkia katika klabu ya Olympique Lyon inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia pound milioni 2.5. 456670762-1-_3212902
Louis van Gaal mbele, nyuma akiwa na beki Rafael August 12 amefunguka na kusema kuwa kilichomtoa hapo ni kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal kutokuwa ana muhitaji na kukiri kuwa kocha huyo hakuwa hakimpenda hivyo hiyo ni miongoni mwa sababu zilizo mpelekea kuondoka klabuni hapo.
rafael-manchester-united_3294598 Rafael alizungumza hayo baada ya kuulizwa kuhusu kuondoka kwake ni kweli Van Gaal hawapendi wachezaji wa kibrazil, Rafael anakiri kusikia hiyo story ya Van Gaal kutopenda wachezaji wa Kibrazil ila hawezi thibitisha kuwa ndio hawapendi ila anachojua hata yeye hakuwa anapendwa na kocha huyo. “Nilisikia hii story ya kuwa hawapendi wachezaji wa Kibrazil lakini siwezi sema hivyo kwani sina uhakika, najua alikuwa hanipendi labda sababu ya mimi kuwa Mbrazil hilo sijui. Nilicheza msimu mzima wa 2012-2013 nikiwa chini ya Ferguson nilicheza kila mechi ulikuwa msimu bora nikiwa Man United kiasi cha kutwaa Ubingwa”>>>Rafael
Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 alicheza kwa miaka saba katika klabu ya Manchester United kabla ya kuondoka wiki iliyopita na kujiunga na klabu ya Olympique Lyon ya Ufaransa, wakati huo Man United ilikuwa ikinolewa na kocha Sir Alex Ferguson.

No comments:

Post a Comment