Popular Posts

Wednesday, 5 August 2015

amaxc blog: huyu ndiye mbadala wa kpah sherman yanga!!!!

Vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu huu vinazidi kujiimarisha kwa kufanya usajili wa mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa August 6, klabu ya Dar Es Salaam Young African imemleta kiungo wa FC Platnum ya Zimbabwe Thabani Kamusoko.
Thabani-Kamusoko Yanga imefanikiwa kumleta Kamusoko ambae amewasili jioni ya August 5 akitokea Zimbabwe na amepokelewa na meneja wa Yanga Hafidh Saleh katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) na kupelekwa moja kwa moja katika kikao na viongozi kinachotajwa kuwa atasaini mkataba wa miaka 2.
ngodzo-kamusoko550 Kamusoko anawasili Dar Es Salaam ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka mshambuliaji wa kimataifa kutokea Liberia Kpah Sherman aondoke na kwenda kujiunga na Mpumalanga Black Aces ya Afrika ya kusini. Dirisha la Usajili litafungwa August 6 na kutakuwa na muda wa wiki moja kwa ajilii ya kuwasajili wachezaji walio huru.

No comments:

Post a Comment