Popular Posts

Thursday, 13 August 2015

amaxc blog: unajua batuli kafunguka inshu flan hv kuhusu siasa!!! kwamba ndo imemfany....

MSANII wa filamu Bongo, Yobunesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa ukimya wake wa kipindi hiki ni kutokana na mambo ya siasa yanayoendelea hivi sasa hivyo ameamua kufunga mdomo wake. Akizungumza na Amani, Batuli alisema kuwa ukimya wake unamsaidia sana ndiyo maana ashabikii upande wowote mpaka maamuzi yatakapotolewa ni chama gani kitatawala nchi yetu. “Mimi sishabikii upande wowote maana haya mambo baadaye yanakuwa mabaya sana, bora mtu unyamaze kimya uone mwisho wake na kitakachoamuliwa na wote ndiyo nitakuwa huko ndiyo maana nimefunga mdomo,” alisema Batuli.

No comments:

Post a Comment