Popular Posts

Saturday, 15 August 2015

amaxc blog:vyombo vya dola vya mkanya mnyika???!!!! jionee full story!!!

Dar/Bukoba. Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limemwonya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kutolihusisha na siasa, huku likikana kuwanyang’anya kadi za kupigia kura maofisa wake ili kufanya hujuma katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Wakati JWTZ likisema hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu amesema suala hilo linapotoshwa na kuwa ni wajibu wa viongozi wa jeshi hilo kuhakikisha askari wote wanatumia fursa ya kumchagua kiongozi wao. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Habari na Uhusiano kwa Umma, Kanali Ngemela Lubinga alisema Jeshi limesikitishwa na kauli ya Mnyika ya kwamba limewanyang’anya kadi za kupigia kura maofisa wake . “Wanajeshi hawaruhusiwi kabisa kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa,” alisema Kanali Lubinga Alisema Jeshi linaendelea na shughuli zake kama kawaida na halitaacha kukemea kauli za upotoshaji zinazolihusu jeshi hilo. Awali, Mnyika alisema Chama cha Chadema kimebaini uwapo wa mbinu za kutaka kuhujumiwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu, kwani Serikali imeviagiza vyombo vya usalama, kupeleka namba za vitambulisho vya askari wote kwa wakuu wa vitengo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.CHANZO:MWANANCHI IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

No comments:

Post a Comment